NIC yatoa mafunzo kwa Mawakala wake wanaotoa Bima za Mali na Ajali

30-05-2022

Author: author

NIC imetoa mafunzo kwa Mawakala wake wa Bima za Mali na Ajali  juu ya masoko na huduma kwa mteja na kuwataka wawe weledi katika utoaji wa huduma. 

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugemzi Mtendaji, Mkurugenzi wa Masoko Bw. Yessaya Mwakifulefule amewataka mawakala hao kuzingatia Mkataba wa Huduma kwa Mteja kila wanapowahudumia wateja kwani kwa kufanya hivyo kutaimarisha ubora wa huduma na kukidhi matarajio ya wateja.